Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Bi.Jesca Msavatavangu akizungumza na wanahabari jioni ya leo mara baada ya tukio hilo la kukamatwa kwa Mbunge wa CHADEMA akigawa fedha kwa wanakijiji siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika. Uchaguzi wa Jimbo hilo unatarajiwa kufanyika kesho siku ya jumapili, ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
 Ikiwa imebaki siku moja kabla ya uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh.Rose Kamili amekamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota, Iringa Vijijini kwa tuhuma za kugawa Fedha kwa wanakijiji hao, akijua fika Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.
Pichani shoto ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Rose Kamili akielekezwa sehemu ya kupita wakati wakiondoka ofisi za makao makuu ya CCM mjini Iringa jioni ya leo,akituhumiwa kukutwa akigawa fedha kwa Wanakijiji wa Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini,ambapo Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.
 Mbunge huyo wa Chadema akipakizwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi kwa taratibu nyingine za kisheria.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh.Rose Kamili akiwa ndani ya gari ya polisi mara baada ya kukakamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini akituhumiwa kugawa Fedha kwa wanakijiji 
Gari ya Polisi PT 1895 ikiondoka na mtuhumiwa huyo,mara baada ya kuchukuliwa kwenye makao Makuu ya chama cha CCM alikokuwa ameshikiliwa na uongozi wa chama hicho,kwa taratibu nyingine za kisheria. PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA-IRINGA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. HA HA HA HA HAHAHAHAHAHAHA NA BADO!

    ReplyDelete
  2. Waliokamatwa wamekatwa na wana CCM. Gari la polisi lilikuwa linafuatilia gari la wana CCM waliokuwa na watuhumiwa. Kama CCM wangekutwa wanotoa rushwa, chadema wangewakamata na gari la polisi kufuatia nyuma? Kulingana na katiba yetu, ni nani aneyeruhusiwa kumkamata mwenzie?

    ReplyDelete
  3. Kwa mujibu wa katiba yetu anaeruhusiwa kumkamata mwenziwe ni wewe mtoa komenti wa pili ambae uko safi na huna dowa .

    ReplyDelete
  4. Hata wewe mwenyewe unaruhusiwa kumkamata mtoa rushwa kwa sababu rushwa hairuhusiwi. CCM ni wapinzani wa CDM lazima waoneshe upinzani wao. Hata CDM wangeona CCM wanafanya hivyo lazima wangechukua hatua sababu hairuhusiwi kutoa au kupokea rushwa.

    ReplyDelete
  5. Chadema chali upende usipende.........Mgimwa ndio huyooooo Mbunge wetu Kalenga Tambarareeee,,,,hureeeeee Kuhonga wamehonga na kura tumempa Mgimwa mpaka rahaaaa....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...