Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kufanikiwa kudhibiti matukio ya vifo na majeruhi katika shughuli za uchimbaji mgodini na kuwasisitiza waajiri wengine kuhakikisha wakati wote wanalinda usalama wa waajiriwa wao.

Biteko ametoa kauli hiyo jana Jumapili baada ya kutembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayoendelea kwenye viwanja vya General Tyre jijini Arusha.

Biteko ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha maonesho hayo, ameeleza kufurahishwa na elimu ya afya na usalama mahali pa kazi inayotolewa na washiriki wa maonesho hayo.

“Niwapongeze wale mliofanya maonesho hapa, mmetoa elimu kubwa kwangu na kwale ambao tumepita lakini tumejifunza bado zipo kazi za kufanya,” alisema.

Alisema waajiriwa wanatakiwa kuzingatia usalama na afya mahali pa kazi kwani kifo cha mtu mmoja kwa takwimu ni sawa na asilimia 100 kwa wategemezi wake ambao ni mke, watoto, ndugu na hata majirani.

“Kifo cha mtu mmoja ni kikubwa kinatakiwa kisitokee. Wito kwa waajiri wote wakati wote nataka mhakikishe mnarekod ziro katika matukio haya ya vifo mahali pa kazi.

“Kwa waajiriwa wito wangu kwenu ni kwamba mtu wa kwanza kulinda usalama ni muajiriwa mwenyewe, ukiona mtambo unaopaswa kuundesha na una kasoro huku ukiwa umelazimishwa na muajiri kuuendesha, uwe wa kwanza kusema mtambo huu haupo salama na usihesabike kuwa mtu uliyegoma kwa sababu pia una wajibu kulinda usalama wako,” alisema.

Alidha alitoa wito kwa kila mtu kuthamini maisha yake kwamba pindi anapokuja kazini anarejea salama bila kuwa na madhara yoyote.

Awali akimkaribisha Dk. Biteko katika banda la GGML, Meneja Usalama wa kampuni hiyo Isack Senya kwa kipindi cha zaidi ya miaka 15 hapajawahi kutokea tukio la vifo kwa mfanyakazi akiwa kazini.

“Tuna miaka zaidi ya sita hakuna mtu aliyeumia akashindwa kurudi kazini siku inayofuata. Suala la msingi tunajitahidi kujifunza kwa wenzetu na kuendelea kuboresha maingira ya afya na usalama mahali pa kazi,” alisema.

Aidha, Senya pia alimueleza Dk. Biteko namna GGML inavyotumia mfumo wa rada kuangalia mienendo ya miamba au kuta katika maeneo ya uchimbaji.

Pia alimueleza kuwepo kwa chumba maalumu cha uokozi ambacho huwepo chini ya ardhi katika migodi ili kufanya uokozi pindi kunapotokea dharura yoyote.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama mahali pa kazi (OSHA), Hadija Mwenda alisisitiza kuwa wataendelea kusimamia majukumu yao ipasavyo kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa.

“Tutaendelea kuhamasisha kuwezesha maeneo ya kazi yawe salama. Suala la usalama na afya ni suala la kujenga tabia na ujengaji tabia ni jambo linatokana na kuelimishwa,” alisema.
 

Meneja Usalama kutoka GGML, Isack Senya (kushoto) akimuelezea Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko namna kampuni hiyo inavyotumia vifaa vyenye teknolojia ya kisasa katika shughuli za uchimbaji ili kuzingatia afya na usalama mahali pa kazi. Anayefuata kulia ni Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi pamoja na viongozi wengine waliotembelea banda la GGML katika maonesho ya Afya na usalama mahali pa kazi yanayoendelea jijini Arusha.

BARAZA la Michezo Nchini (BMT) La ahidi kushirikiana bega kwa bega na Shirikisho la Mbio za Magari (AAT) Kuhakikisha wadau wanaunga mkono mchezo huo.

Akizungumza na Wadau na Wachezaji wa Mashindano ya mbio za magari wakati wa Kugawa tuzo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la michezo (BMT) Neema Msitha amesema amefarijika kuona Shirikisho la Mbio za Magari (AAT)Wamekumbuka na kuwakutanisha wachezaji wa Mashindano haya ya magari na kufanya hivyo ni kuwatia Moyo ili kufanya vizuri zaidi hivyo nafasi ya ushindani itaendelea kuwepo.

Aidha amesema Lengo la Serikali ni Kuona michezo inaendelea kupaa zaidi endapo mtu mmoja mmoja hatotambua nafasi yake .

"Zinapokuwepo Medali au nishani inawasaidia wachezaji hao kuendelea kufanya vizuri ndani na nje ya nchi na kuitambulisha nchi ya Tanzania katika michezo.

Pia ametoa wito kwa Shirikisho la mbio za magari (AAT) kutafuta wadau ambao watawekeza katika mchezo huo na kuendelea kuibua vipaji mbalimbali kama michezo mengine.

Aidha Kwa Upande wake Rais wa Shirikisho la mbio za Magari (AAT) Nizar jivan amesema Chama hicho Kitaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa kuendelea kuwepo kwa Mafunzo ya Usalama Barabarani Nashuleni kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

"Chama hichi kimekuwa kikishirikiana kwa karibu na Serikali na tumekuwa tukijitolea kwa kuwafata Wanafunzi mashuleni kuwapa mafunzo ya usalama barabarani na kuboresha miundombinu ikiwemo kuweka vivuko barabarani maeneo karibu na shule za Misingi."

Hata hivyo amesema tuzo hizo zitaendelea kutolewa kila mwaka ili kuwatia moyo wachezaji hao wa mbio za Magari nchini sanjari na Mafunzo mbalimbali yanaendelea kutolewa kwa lengo la usalama barabarani kwa wachezaji hao.

Pia ametoa wito kwa washini wote waliofanikiwa kupata Tuzo kuendelea kushiriki mchezo huo kwa usalama kwani imejengeka desturi kuwa mchezo ni hatari na unapoteza maisha kwa haraka zaidi.
 

Katibu Mtendaji wa Baraza la michezo (BMT) Neema Msitha akikabidhi Kikombe Kwa Mshindi dereva bora Mr.Birdi  katika hafla ya Tuzo za Usiku wa Mabingwa wa Mashindano ya mbio za Magari Jijini Dar es Salaam
 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo (BMT) akizungumza na Wadau wa Mashindano ya Mbio za Magari wakati wa Tuzo zao Jijini Dar es Salaam ambapo amewataka wachezaji hao kutafuta wadhamini ili kuendeleza mchezo huo
 

Mwenyekiti wa Shirikisho la mbio za magari (AAT) Satinder bird akiwa na Washindi wa Mashindano ya Mbio za Magari kutoka Klabu mbalimbali sherehe iliyofanyika Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024. Rais Samia anatarajia kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA. IDA ni Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia unaotoa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024. Rais Samia anatarajia kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA. IDA ni Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia unaotoa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha (kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili Jijini Nairobi Kenya tarehe 28 Aprili, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Ua mara baada ya kupokelewa na Watanzania Waishio Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na baadhi ya Watanzania waliofika kumpokea Jijini Nairobi mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha (kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA

Na. Josephine Majura na Saidina Msangi, WF, Nairobi, Kenya

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), ameungana na Mawaziri wa Fedha wa Afrika kushiriki katika mkutano maalum wa kujadili vipaumbele vya Afrika ili viweze kuzingatiwa katika maandalizi ya Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maaalumu wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) unaotarajiwa kuanza Julai 2025 – Juni 2028.

Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya. ni utangulizi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21, utakaofanyika tarehe 29 Aprili mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano huo Dkt. Nchemba, alisema kuwa Tanzania imeungana na Mawaziri wengine katika kuhakikisha kuwa inasisitiza umuhimu wa kuongezewa fedha za dirisha la 21 la IDA ili kuweza kuchangia katika utekelezaji wa ajenda na malengo ya maendeleo ya Bara la Afrika.

“Hili dirisha limekuwa likitoa mikopo kwa masharti nafuu, riba kwa kiwango cha chini na muda wake wa kurudisha umekua mrefu ambapo Tanzania kwa kiwango kikubwa imekuwa ikitumia dirisha hilo kupata fedha ambazo zimekua zikitumika katika kuendeleza sekta za huduma za jamii kama vile elimu, maji pamoja na umeme kwa bei nafuu”, alisema Dkt. Nchemba.

Alifafanua kuwa dirisha hilo ambalo riba ya mikopo yake haizidi asilimia mbili limekuwa likitoa mikopo kwa nchi za Afrika yenye masharti nafuu ili kuzipunguzia nchi hizo kupata mikopo kutoka benki za kibiashara ambayo huwa na gharama kubwa.

Aidha, Dkt. Nchemba alisema kuwa mkutano huo utasisitiza umuhimu wa kupatikana kwa fedha za IDA kwa ajili ya kuzisaidia nchi kutoka katika athari za majanga na kuwezesha kurejea katika hali ya kawaida kwa ajili ya maendeleo endelevu Afrika.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El Maamry Mwamba, Kamishna wa Fedha za Nje Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Yussuf Ibrahim Yussuf na viongozi wengine wa Wizara.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), akipokelewa na Waziri wa Fedha wa Kenya Prof. Njuguna Ndung’u, alipowasili kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika tarehe 28 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El Maamry Mwamba, (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Kenya Dk. Chriss Kiptoo, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika tarehe 28 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya.


Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), akisalimiana na Waziri wa Mipango Angola Victor Hugo Guiherme, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika tarehe 28 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, jijini Nairobi, Kenya.



 

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), akiteta jambo na Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Enoch Godogwana, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika tarehe 28 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya.


 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, na Kamishna wa Fedha za Nje Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Yussuf Ibrahim Yussuf (katikati) na  Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe. Balozi Noel Kaganda, wakiwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika tarehe 28 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, jijini Nairobi, Kenya.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Nairobi, Kenya)

UTOAJI Wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi inayotolewa bure kwa wasichana kuanzia miaka 9 hadi 14 kwa dozi moja pekee umefanikiwa kwa asilimia 95 tangu kuanza kutolewa kwake Aprili 22, 2024.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Mpango wa Chanjo wa Taifa; Dkt. Florian Tinuga jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo maalum kwa waandishi wa habari yaliyolenga kuwajengea uwelewa zaidi kuhusu chanjo hiyo ya Human Papilloma Vaccine (HPV,)

“Tangu kuzinduliwa kwake mwezi Aprili mwaka huu wasichana walengwa asilimia 95 wamefikiwa na chanjo hii ambayo Wizara ya Afya kupitia Mfuko wa Taifa wa Chanjo ililenga kuwafikia na kuwapa chanjo wasichana 187,059 kutoka visiwani Zanzibar na 4,841,298 kutoka Tanzania Bara ambao wamefikisha umri wa miaka 9 hadi 14.” Amefafanua.

Aidha kuhusiana na mabadiliko ya dozi ya chanjo hiyo kutoka dozi mbili hadi moja Dkt. Tinuga ameeleza kuwa mwaka 2023 Kamati ya Kitaalam ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu Masuala ya Chanjo ilifanya utafiti na kujiridhisha juu ya ubora na usalama wa dozi moja ni sawa na dozi mbili katika kutoa kinga ya mwili dhidi ya kirusi dhidi ya kirusi cha HPV.

“Utafiti wa kisayansi kuhusu usalama wa dozi moja ni matokeo ya tafiti za kisayansi za ubora na usalama wa dozi moja kwa wasichana zilizofanywa na wataalam wetu pamoja na muongozo uliotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO,) mwaka 2022 ambalo pia lilithibitisha ubora na usalama wa chanjo moja na kutoa uamuzi kwa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kutoa dozi moja ya kuwakinga wasichana dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi…” Amesema.

Amesema kuwa mwitikio wa wasichana wa umri lengwa kwa ajili ya kumkinga binti dhidi ya maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi ni mkubwa kutokana na ushirikiano na wadau mbalimbali hususani Wizara ya Elimu pamoja na wazazi na walezi kwa kuwa chanjo hizo hutolewa shuleni na katika vituo vya huduma za chanjo katika vituo vya Afya.

Amesema saratani ya mlango wa kizazi husababishwa na kirusi cha papilloma na huambukizwa kwa njia ya kujamiiana na wanaume ndio hubeba kirusi hicho na mwanamke kupata madhara zaidi huku dalili zake zikiwa ni pamoja na kupata hedhi isiyo na mpangilio maalum na kutokwa na uchafu au damu ukeni huku Mikoa ya Kilimanjaro, Dar es Salaam na Mwanza ikiongoza kwa saratani hiyo.

Imeshauriwa kuwa ni vyema wasichana wa umri wa miaka 9 hadi 14 kupatiwa chanjo hiyo kwa kuwa imethibitika kisayansi katika umri huo mwili una uwezo wa kujitengenezea kinga ya kutosha, kuepuka ngono katika umri mdogo pamoja na kufanya uchunguzi kila baada ya miaka mitatu hadi mitano ili kufahamu dalili za awali na kuwahi tiba.
 

Meneja wa Mpango wa Chanjo wa Taifa Dkt. Florian Tinuga (kulia,) akitoa mada wakati wa mkutano huo na kueleza kuwa chanjo ya HPV ni salama kwa kinga mwili dhidi ya kirusi cha papilloma kinachosababisha saratani ya mlango wa kizazi.



 

Matukio mbalimbali wakati wa mkutano huo.

Serikali imetoa shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kuanza urejeshaji wa miundombinu ya barabara zilizoharibika maeneo mbalimbali Mkoani Mwanza.

Fedha hizo zimetolewa na serikali kwenda Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mwanza ili kuanza haraka kazi ya marekebisho miundombinu ya barabara na madaraja ambayo yameharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha

Meneja wa TANROADS Mkoa Wa Mwanza Mhandisi Paschal Ambrose ameyasema hayo wakati alipotembelea na kukagua uharibifu uliotokea kwenye barabara katika Wilaya za Nyamagana na Misungwi ambapo pia ametumia fursa hiyo kukanusha uvumi ulioenezwa kwamba barabara katika eneo la Ng'ombe Wilayani Misungwi ni mbovu na haipitiki na amewataka wananachi kupuuza uvumi huo.

Amesisitiza kuwa Serikali imetoa fedha za dharura ambapo tayari wakandarasi wapo kazini wakiendelea na kazi.

Amesema miongoni mwa barabara zinazofanyiwa marekebisho ni barabara ya kutoka Mwanza kuelekea Musoma eneo la Nyamhongolo ambapo wanarekebisha mfereji ambao umeharibika kutokana na mvua hizo.

Mhandisi Ambrose amewataka wananchi wanaoishi karibu na barabara kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye kingo za barabara pamoja na kutupa taka ngumu katika mitaro hali inayosababisha mitaro kushindwa kupitisha maji pindi mvua zinaponyesha.

Naye Mkandarasi anayefanya marekebisho katika maeneo mbalimbali Mkoani Mwanza Mhandisi Stephen Mashauri kutoka kampuni ya ujenzi ya MUMANGI CONSTRUCTION CO. LTD amewaondoa hofu wananchi wanaotumia barabara hizo kwamba zitarekebishwa kwa wakati ili ziweze kupitika muda wote.

Aidha amewataka madereva wa vyombo vya moto kufuata alama zote, za barabarani zilizowekwa na TANROADS ili kuepuka ajali, huku akiwatahadharisha Wananchi wanaoiba miundombinu iliyowekwa barabarani na kwamba watakaobainika watachukulia hatua kali za kisheria.








Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Taasisi zinazoshirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kutekeleza masuala ya local content.

Kufuatia ushindi huo, PURA imekabidhiwa tuzo maalum wakati wa hafla ya kuhitimisha Kongamano la Nne la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati iliyofanyika Aprili 28, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Akitoa maelezo ya Kamati ya kujitegemea iliyoundwa kuratibu mchakato wa tuzo hizo, Mwenyekiti wa Kamati Bw. Christopher Mushi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI alieleza kuwa ushindani ulifanyika kwa kuzingatia vigezo vya kila kundi.

"Kila kundi lilitakiwa kuwa na washiriki wasiopungua watano na washindi wa kila kundi walitakiwa kupata alama za ufaulu zisizopungua asilimia hamsini" alifafanua Bw. Mushi.

Tuzo zilikabidhiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuhitimisha Kongamano hilo.


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko (kushoto) akikabidhi tuzo kwa PURA baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza katika kundi la Taasisi zinazoshirikiana na NEEC kutekeleza masuala la local content. Anayepokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PURA ni Bw. Charles Nyangi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wazawa na Uhusishwaji wa Wadau kutoka PURA. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa halfa ya kuhitimisha Kongamano la Nne la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika miradi kimkakati iliyofanyika Aprili 28, 2024

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko (kushoto) akikabidhi tuzo kwa PURA baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza katika kundi la Taasisi zinazoshirikiana na NEEC kutekeleza masuala la local content. Anayepokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PURA ni Bw. Charles Nyangi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wazawa na Uhusishwaji wa Wadau kutoka PURA. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa halfa ya kuhitimisha Kongamano la Nne la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika miradi kimkakati iliyofanyika Aprili 28, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndugu Winfrida Beatrice Korosso kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndugu Bibiana Joseph Kileo kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Aprili, 2024.
Ndugu Bibiana Joseph Kileo Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Ndugu Alice Edward Mtulo Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na Ndugu Winfrida Beatrice Korosso Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakiapa Kiapo cha Maadili ya Viongozi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango wakiwa katika picha ya pamoja na Ndugu Bibiana Joseph Kileo Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Ndugu Alice Edward Mtulo Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na Ndugu Winfrida Beatrice Korosso Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania mara baada ya hafla fupi ya kuwaapisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Aprili, 2024.

Zanzibar: Najjat Omar.
CHAMA Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania -Zanzibar – TAMWA-Z kimekutana na waandishi wa Habari chipukizi,wahariri,wamiliki wa vyombo vya Habari na wadau wa Habari kwa kuwatunuku na kuwatunza waandishi wa Habari 23 waliokuwa kwenye mradi wa Waandishi Chipukizi.

Mahafahali hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Bima uliopo Maisara Mjini Magharib Unguja.

Khairat Haji ni Kaimu Afisa Programmu TAMWA -Zanzibar amesema katika hatua za kumarisha uongozi kwa wanawake ,mradi huu ambao hii ni awamu ya pili ambapo kwa awamu ya kwanza uliwafunza na kuwasimamia waandishi vijana 18 kwa 2022 .Huku mwaka 2023 waamdishi vijana 24 walipata fursa katika mradi huu wa Wamawake na Uongozi”Kupitia mradi huu ulikuwa unahitaji kazi 348 na hadi kufikia leo kazi hizo ni 347,huku magazeti 47 ,Makala za radio 117 huku Makala za mitandamo 187 ambazo zinakamilisha kazi 347” Amesema Khairat

Shifaa Said ni Jaji Kiongozi wa Tuzo za Waandishi wa Habari Chipukizi kwenye kuhariri kazi za waandishi hao 24 zilizofika kwao kazi hizo ambazo zimehaririwa kwa siku nne ,kazi hizo ambazo zilikuwa ni 175 kati ya hizo magazeti ni 15 za radio 85 na mitandao ya kijamii 75.Amesema “Vigezo muhimu vilivyozingatiwa kwenye kazi hizo ni Pamoja na weledi na umahiri katika sauti pamoja na sauti zizosikika huku upekee wa mada na kuangalia kuwafikia watu wenye mahitaji maalum” Amesema Shifaa Said.

Akiongeza kuwa “Mafanikio na ukuwaji wa wanufaika wa mradi huu kwa mwaka huu wameweza kuandika na kuchapisha Makala na vipindi vyema mabadiliko kwenye jamii” Amemaliza Shifaa Said.

Hawra Shamte ni Mjumbe wa Bodi ya Tamwa Zanzibar,amesema kuwa kuwepo kwa mahafali hii leo ambao wamepata nafasi ya kuwa kwenye huu kukubali kujifunza na kuandika masuala ya wanawake na hii ni “Dhahiri kuona kwamba majukumu yenu kwenye kuandika masuala ya wanawake na uongozi yametamalaki na ni hakika tuendelea kaundika na kuuhabarisha umma juu ya uwepo kwa habari hizi katika kuleta mabadiliko katika jamii hii ambayo inategemea kuwa na viongozi wanawake na wanaume.” Amesema Hawra.

Akiwa mmoja wa wanufaika kwa mradi huu Berema Suleiman Nassor ni mwandishi wa Zenji Fm pia ni mnufaika wa Mradi huu amesema kwenye uandishi wa Makala za wanawake na uongozi suala la upatikanaji wa data ni changamoto. Huku Nihifadhi Abdulla ambaye ni mwandishi wa Kati Fm amesema kuwa zamani alikuwa akiiandika Makala na Habari za kawaida ila sasa amebadilika “Sasa naandika habari zenye kuleta mabadiliko na usawa wa kijinsia kwanza sikuweza ila kwa sasa naona kwamba nimekuwa na naweza kupikwa vyema” Amemaliza.

Salma Said ni Mwandishi wa DW na Mhariri na amesema suala la kuona vijana wanakuwepo kwenye mradi huu ni kuonesha masuala ya uandishi wa Habari za viwango na wenye kuleta mabadiliko “Ikiwa haya yataendelea kuandikwa basi kutakuwepo na mabadiliko katika jamii kwenye uleta uwajibikaji ,kubadilishwa kwa sheria na haki kutendeka” Amesema Salma Said wakati akizungumza kwenye Mahafali hayo.

Issa Yussuf ni Mwandishi wa Gazeti la Daily News amesisitiza matumizi ya lugha ni muhimu sana kwenye uandishi wa Habari “Masuala ya lugha kwa usahihi na usanifu ni jambo ambalo litawafikisha mbali na kuwasaidia zaidi kwenye uandishi wa kujifunza na kusoma masuala ya mikataba na sheria mbali mbali.” Amesema Issa.

Akitoa Tuzo na kwa waandishi hao Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania -Zanzibar TAMWA -Zanzibar.Dkt Mzuri Issa amesema “Kuwa makala hizi kazi hizi zimeleta mabadiliko kwenye jamii kwa kuwashawishi wanawake kuingia kwenye siasa na kupata nguvu ya kusaidia kuvunja dhana potofu kwenye ya kuwa wanawake hawezi kuwa viongozi kuwa kwenye uongozi.” Amemaliza.

Mradi huu wa wanawake na Uongozi uliotekelezwa na TAMWA Zanzibar kwa kushirikiana na shirika la National Endowment for Democracy (NED) wa kuwawezesha waandishi wa habari vijana YMF kuandika habari za wanawake na uongozi umewashirikisha waandishi vijana ishirini na nne (24) kutoka Unguja na Pemba.

Kaimu Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya UNESCO Tanzania Fatuma Mrope wa kwanza kutoka kulia akikabidhi cheti Mnufaifaika wa Ufadhili wa Masomo nchini Poland George Kato wa tatu kutoka kushoto katika makabidhiano yaliyofanyika katika Ofisi ya Tume hiyo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya UNESCO Tanzania Fatuma Mrope wa kwanza kutoka kulia akikabidhiwa baadhi ya taarifa na Mnufaifaika wa Ufadhili wa Masomo nchini Poland George Kato wa tatu kutoka kushoto katika makabidhiano yaliyofanyika katika Ofisi ya Tume hiyo jijini Dar es Salaam.

*Miradi ya Kimkakati ni fursa ya kwenda kupata ufadhili na kuongeza maarifa

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
VIJANA  nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za kusoma nchi nchi zinazotolewa Tume ya Taifa ya UNESCO kutoka nchi wafadhili.

Tume ya Taifa ya UNESCO Tanzania imekuwa inapata ufadhili wa vijana katika kusoma nchi mbalimbali lakini changamoto iliyopo ni vijana kutoomba nafasi hizo za kusoma.

Hayo ameyasema Kaimu Katibu mtendaji mkuu wa Tume Fatuma Mrope amesema kuwa nafasi zipo nyingi za kusoma katika nchi za Poland ,China na nchi nyingine.

Amesema Teknolojia zinabadilika kila siku katika program za kusoma ambapo nchi ambazo zinatoa ufadhili zimefika mbalimbali ambapo kwenye miradi ya kimkakati inayofanyika nchini wanaweza kutumika kuliko kutafuta nje ya nchi hizo zilizoweza kuwa Teknolojia hizo na zikatoa ufadhili.

Kaimu huyo Fatma amesema kazi ya UNESCO ni kutafuta nchi zenye utayari wa kutoa ufadhili kwa vijana nchi za Afrika katika shahada ya kwanza,Shahada ya pili pamoja na shahada Uzamivu (PhD) na kuzitangaza kwa watanzania ili waweze kuomba na kunufaika nazo.

Akielezea utaratibu ulivyo Afisa Program wa UNESCO Tanzania Adrian Hyera amesema ufadhili unaotolewa ni bure na kazi kubwa kwa wanahitaji ni kuomba kwenye tovuti za Tume ya Taifa UNESCO Tanzania.

"Nchi nyingi fursa ufadhili wa kusoma wanazitumia zikifika Tanzania vijana hawaombi hadi program za nchi zilitoa ufadhili zinaisha"amesema Hyera

Aidha amesema kuwa ufadhili huo licha ya kuwa bure ni bure kwa kipindi unachokuwa unasoma na gharama zinazomhusu kama mwanafunzi ni kusoma tu.

Hyera amesema kuwa vijana wanaotaka kupata ufadhili nafasi ziko za kutosha kwani idadi wakati mwingine wanatakiwa 10 nchi lakini Tanzania unakuta hata kijana mmoja hajaenda.

Mmoja wa Wanufaika George Kato aliyekwenda kusoma utalii wa Miamba nchini Poland amesema kuwa kwa Tanzania alikuwa pekee yake huku baadhi ya nchi zikiwa zina zaidi ya watano.

Kato amesema kuwa haoni sababu ya vijana kushindwa kutumia fursa wakati kwao inaongeza utaalam wa kufanya kuingia katika ushindani wa soko la ajira.

Amesema kuwa wakati alipoenda ofisi za Tume ya Taifa ya UNESCO Tanzania alipata msaada mkubwa hadi kukamilisha taratibu na kwenda kusoma katika nchi hiyo.

 Na Mary Margwe, Simanjiro.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Maryam Muhaji ameitaka jamii kuhakikisha wanaimarisha Muungano huo, pamoja na kukemea vitendo vya Ukatili wa Kijinsia vinavyoendelea katika Mkoani humo.

Kufuatia kuwepo kwa vitendo hivyo ndani ya Mkoa huo amewaomba viongozi wa Dini katika Makanisa na misikiti suala la Ukatili wa Kijinsia iwe ndio agenda ya kukemea ukatili wa kijinsia.

" Wana Manyara ni wazuri sana isipokua  lakini tunaharibiwa  na huu ushwerati ambao umetutawala kwenye suala Zima la Ukatili, hivyo Viongozi wa Dini niwaombe kulitenda hili Kwa haraka zaidi ili liweze kuwa na mwitikio mzuri kwa jamii.

Naye Katibu wa Siasa ,  Itikadi na na   Mafunzo Mkoa wa Manyara  John Nzwalile amesema zipo faida nyingi za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na hivyo kuwaomba Watanzania kutoruhusu watu kuubeza Muungano huo.

Nzwalile amesema Muungano ndio maisha, Mafanikio yote yanayoonekana yamefanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si vinginevyo.

" Naomba Watanzania wasiruhusu watu kuubeza Muungano wetu huu, Muungano wetu huu ndio maisha yetu, Mafanikio yote unayoyaona yamefanywa  na Serikali  yetu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kwasababu ya utulivu, amani na Usalama iliyowekwa na viongozi wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania " amefafanua  Nzwalile.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT ) Wilaya ya Simanjiro Anna Shinini amesema Muungano huo umeendelea kuwaunganisha akina mama Kwa Umoja wao na kuwapa nguvu,  ujasiri mkubwa wa kufanya kazi hususani kupitia nafasi ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan kama mwanamke shupavu, Mahili katika kuliongoza Taifa  Kama Rais

" Siku ya leo na Mimi kama Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Simanjiro namuunga mkono mama yetu Mchapakazi Mh. Samia Suluhu Hassan ambaye ni mwanamke aliyetujengea ujasiri mkubwa na sisi tunamuumga mkono kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuendelea kumtia moyo katika Utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku,  amesema Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Simanjiro 

 Aidha Shinini amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kurudisha mikopo ya asilimia 10 iliyokua ikitolewa katika kila Halmashauri hapa Nchini kupitia mapato yake ya ndani, ni mikopo iliyokuwa na msaada mkubwa sana kwa walengwa katika kuwaondoa katika wimbi la u amaskini na kuwainua kiuchumi.

" Nimefurahi sana leo kusikia ile mikopo ya asilimia 10 imerudi, kwani ilikua ndio nguzo muhimu ya kumkomboa mwanamke, vijana na Watu wenye ulemavu na hatimaye kuwakomboa kwenye wimbi la umaskini, kwani mikopo ya nje ya Serikali baadhi  imekua ni mikopo kandamizi Kwa kuwa na riba kubwa iliyowapelekea hata baadhi yao kufilisiwa mali zao kwa kushindwa kurejesha marejesho.

Aisha SHININI amesema Mikopo hii ilishakuwepo ambapo Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu walikua wakinufaika nayo kwani Serikali imekua ikitoka mikopo hiyo hiyo bila riba ili kuwawezesha kuinua uchumi na hivyo kuwawiaburahisi kuwaletea Maendeleo ya haraka, ukilinganisha na hiyo mikopo mingine.


"  Sasa  wanaendelea kupata mikopo, tunamshuku sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kurudisha mikopo hii ambayo itawasaidia kuwainua kiuchumi na hatimaye kuweza kuondokana na umaskini, kikubwa ni umaminifu wa kuchukua fedha na kurudisha" 

Kufuatia hilo pia amewataka wanaochukua mikopo kuweza kuhakikisha mikopo wanayoichukua inawanufaisha kisawa sawa ikiwa ni sambamba na kurudisha fedha hizo Kwa wakati  ili iliwe kuwasaidia na wengine

Aidha amewataka wanawake  pamoja na wananchi wote Kwa ujumla kuhakikisha wanamuunga mama mkono kwasababu Muungano wetu ni kioo, ni dira ndani ya nchi yetu ndio inayotuonyesha tumetoka wapi, tuko wapi na tunatarajia kufika wapi, na hivyo Rais Samia anatupa nguvu zaidi kuweza kufanya kazi ndani ya Taifa letu.



Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe.Daniel G. Chongolo ameshiriki katika ibada maalumu ya Kanisa la KKKT Jimbo la Tunduma ikiongozwa na Askofu Mkuu wa makanisa ya KKKT Tanzania Dkt. Alex Malasusa iliofanyika katika mji wa Tunduma sambamba na uzinduzi wa ukumbi wa kanisa hilo.

Akiongea katika hafla hiyo Chongoloa amesema mkoa wa Songwe ni moja kati ya mikoa mikubwa na inayosifika kwa kilimo lakini cha ajabu ni moja ya mikoa yenye changamoto ya lishe hivyo amemuomba askofu Malasusa kupitia kaanisa la KKKT Jimbo la Tunduma kuhakikisha wanahubiri pia lishe ili kunusuru Mkoa na janga la udumavu

Aidha pia mkuu wa mkoa alimueleza askofu na waumini walioshuhudia uzinduzi huo jambo lingine linausumbua mkoa wa Songwe ni tatizo la mimba za utotoni na ndoa za utotoni hivyo amewaomba waumini wa KKKT kuisaidia serikali katika kukemea vitendo hivyo na kushiriki katika Malezi Bora ya watoto wetu

Akimalizia hotuba yake Chongolo amekemea vitendo vya mauaji kukithiri ndani ya maeneo mbalimbali ya mkoa.

Kwa upande wake Askofu Malasusa amesema mkoa wa Songwe umempata mkuu wa mkoa mchapa kazi kweli na anayesikia ushauri hivyo ameomba waumini wamuombe ili kazi yake iweze kuwa rahisi na bila kusahau awe msaidizi mzuri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani ambae amemuamini kumleta Songwe amsaidie

Askofu amesema yale yote yaliosemwa na RC Chongolo yote pia ni majukumu ya Kanisa hivyo amewaleza waumimi wa KKKT Tunduma kuwa suala la lishe na malezi ni moja ya majukumu ya Kanisa na ni sehemu ya kuheshimi uumbaji wa Mungu na kutukuza hivyo jukumu la malezi na lishe .

Pia Malasusa ameagiza kila baraza la wazee Jimbo la Tunduma KKKT wanapokutana wawe wanajadiliana juu ya lishe na malezi ya watoto

Akimalizia Malasusa amekea pia vitendo vya mauaji na kusema hata Mungu vitendo hivyo havimfurahishi na ni kumuingilia Mungu majukumu yake hivyo amewaomba waumini kumrudia Mungu na kufuata makatazo yake ndani ya Biblia

Mkuu wa Mkoa Chongolo amechangia kiasi cha shilingi Milioni moja kama mchango wake wa awali wa kukamilisha Ujenzi wa Ukumbi huo.





Top News